Luke 12:40-45

40 aNinyi nanyi hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.”

Mtumishi Mwaminifu Na Yule Asiye Mwaminifu

(Mathayo 24:45-51)

41Ndipo Petro akamuuliza, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?”

42 bIsa akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa? 43Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44 cAmin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 45 dLakini kama yule mtumishi atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa.
Copyright information for SwhKC